Wabaptist na Huduma ya Kuhudumia Wahitaji

“…Kadri mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”
Mathayo 25:40

Njia moja wapo ambayo Wabaptist wanaendelea kuishi sawa na ima ni yao ni kutoa huduma za mahitaji kwa wahitaji. Kwa njia zote mbili kwa ulimwengu kote, Wabaptist hugusa mioyo ya watu kwa njina la Yesu.

Msingi wa Huduma kwa Wahitaji

Msingi wa Baptist juu ya kutoa huduma kwa wahitaji chanzo zhake ni mafundisho na desturi za Kibaptist.  Hiyo huduma sio kwamba imevamiwa tu bali ina maana kuwa ya kuonyesha Wabaptist wakoje. Sababu ya kusema, kuwa na hiyo na uwepo wa hii huduma yote ni kuhusiana na msingi na imani ya Wabaptist.

Wabaptist husisitiza ukuu wa Yesu Kristo. Bwana Yesu alitoa wito kwa watu wake kuhudumiana.

Yesu alionyesha mfano kupitia huduma yake kwa kuwahurumia watu wote na kuwapatia mahitaji yao ya msingi yote.  Kuonyeshwa kuguswa na mahitaji ya watu wake, aliwafanya vipofu kuona, viwete kutembea na wagonjwa kuponywa (Mathayo 11:5). Aliwafanya watu waliopoteza akili na afya kurudi kwenye hali zao za kawaida. Aliwaheshimu watu na hali zao na kuwakubali watu wenye tabaka mbalimbali mfano watozwa ushuru na mwanamke mzinifu.

Zaidi ya hapo, Yesu kama Bwana alifundisha umhumimu wa hii huduma.  Aliwaambia wanafunzi wake, “hivyo watu watatambua, mnao upendo ninyi kwa ninyi” (Yohana 13:35).  Alipoulizwa kuwa amri mkuu ni ipi, alisema ni mbili: kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako (Mathayo 22:37-40). Kumpenda jirani yako, Yesu alisema, ni pamoja na matendo ya kumpatia mahitaji yake. Alisema msingi wa hukumu ya milele uko kwenye kusema ni jinsi gani watu wameweza kutimiza mahitaji ya watu wengine(Mathayo 25:31-46).

Wabaptist bado wamejikita kwa kuitambua Biblia kama ndiyo yenye mamlaka  juu ya imani na mwenendo.  Biblia inatufundisha wazi umuhimu wa huduma ya kuwasaidia wengine. Biblia inatufundisha  tunapaswa kuwa na upendo na sio wa maneno tu bali hata kwa matendo na kuwa na huruma kwa mahitaji ya wengine (1 Yohana 3:17-18).  Agano Jipya linatufundisha ni jinsi gani mapema Makanisa ya kwanza yalifanya hilo.

Wabaptist huamini kwamba wokovu huja kwa njia ya imani baada ya kukubali kuipokea neema ya Mungu ya wokovu kupitia Yesu. Hatuokolewi kwa matendo mema bali tunaokolewa kwa njia ya imani. Hata hivyo, wokovu unapaswa kuonyesha matunda ya matendo mema: “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema.” (Waefeso 2:10), “Imani bila matendo imekufa, Biblia inafundisha (Yakobo 2:20).

Wale wanaokolewa kupitia imani kwa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi hufanyika  makuhani waumini  (1 Petro 2:5; Ufunuo 1:6). Kila kuhani muumini anao wajibu wa kuwahudumia wengine. Kusaidia wahitaji sio tu ni jukumu la Wachungaji na Mashemasi lakini ni kwa ajili ya wote makuhani waumini. Walikutana na changamoto mbalimbali na huhitaji msaada, makuhani waumini wanapaswa kuonyesha kwa njia ya uweza wa ili kuona na kufuata kusudi la Mungu kwa kuona ni mahitaji gani yanapaswa kufikiwa. Katika hili, hutegemea nguvu (Matendo 1:8) na uongozi wa Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:25).

Desturi za Wabaptist uongozi shirikishi wa Kanisa la mahali, kujitegemea kwa Kanisa la mahali na uhiari wa ushirikiano. Dhehebu la Baptist haliwezi – na halitaweza – kuliamrisha Kanisa la mahali ni huduma gani ya kusaidia wahitaji inaweza kuifanya au jinsi gani ya kushirikiana kwenye hii huduma na wengine. Kanisa linafanya huduma mbalimbali. Na hufanya kwa umoja kwa hiari kupitia kazi za majimbo, kanda, ngazi ya taifa, taasis na kwenye umoja wao.

Kuimalika kwa nguvu  kwa uhuru wa kuabudu  kumewafanya Wabaptist kufanya shughuli zao mbalimbali bila kushinikizwa. Watu na Makanisa yako huru kuchangua ni huduma gani ya kufanya. Hizi huduma huendeshwa kwa njia ya kutoa kwa hiari kwa waumini wa Baptistas (2 Wakorintho 8:1-8),  sio kwa mapato ambayo hupatikana kwa kutozwa kodi, au ruzuka ya dhehebu, hayo yote mawili yanaweza kuachilia suala la kusukumwa kufanya.  Huduma ya kusaidia wahitaji ndani ya Baptist imejikita kwenye kujitolea, msaada wa hiari na ushiriano wa hiari.

Kiwango cha huduma

Kiwango cha huduma hii kwa Baptist ni kutokana na mfano na mafundisho ya Yesu na maelekezo mengine kwenye Biblia. Hivyo basi, huduma hii ni ya kinadamu ajili ya watu, na watu wote kokote waliko wenye uhitaji.

Ubinadamu  ndilo kusudi kuu la huduma hii ndani ya Baptist – kiroho, kimwili, kiakili, kimawazo na majitaji ya kijamii. Mahitaji ya kimwili hupatikana kutokana na huduma hizo kama vile chakula, maji, makazi na matibabu.  Mahitaji ya kiakili na mawazo  hupatikana kwa njia ya ushauri nasaha, kuwatembelea wenye shinda na kuhubiri na kufundisha.  Mahitaji ya kijamii  hupatikana kwa kuwa na ushirika, burudani, kujumuisha na watu wenye msongo wa mawazo na waliojitenga kwenye haya matukio na mengine. Mahitaji ya kiroho  hushughulikia kwa njia ya uinjilisti, umisheni, uanafunzi na elimu ya Kikristo.

Wabaptist hawaoni msaada wa kimwili kuwa ndio suluhisho bila kuwepo msaada wa Kiroho ndani yake, kama vile kuwa na sehemu ya uinjilisti na ushauri wa Kikristo.

Wabaptist pia hutoa huduma  kwa watu wote —watu wenye rika zote, yote uanayohusiana na kiroho, yote ya mwilini, yote ya mawazo na kiakili; makabila yote, tamaduni zote, hali za maisha zote, wasomi na wenye viburi, hali zozote za uwezo wa kiuchumi, elimu na hali za jamii husika.  Huduma za Kibaptist   zinapatika kwenye maeneo mablimbali. Iwe mjini, magerezani, kambi za kijeshi, hospitalini, maeneo ya vijijini, kambi za wakimbizi, maeneo ya majanga mbalimbali…. Wapi na wapi orodha inaendelea mahala ambako Wabaptist huenda na kutoa huduma za msaada. Hizi huduma za kuhudumia jamii za Kibaptist zipo mahali husika, kwenye mikoa, kwenye taifa na maeneo yeyote ulimwengu mzima.

Njia za Kutoa Huduma

Huduma hizi za kusaidia jamii kutolewa kwa njia mbalimbali. Hizi njia hufanikisha na watu, Makanisa, mashirika, na taasis za dhehebu ndani ya Baptist kama vile majimbo na Kanda.

Kwa kufuata mfano na mafundisho ya Yesu,  Watu binafsi wa Kibaptist huhudumia watu wenye uhitaji, wao kama wao, kuliko nguvu kutoka kwenye taasis yeyote, Wabaptist huganga vidonda vya walioumia, kutembelea wagonjwa na wafiwa, kutia moyo walioumizwaa na kufanya huduma zingine nyingi za kusaidia. Zaidi ya hayo, watu waliojitoa kikamilifu wanaunda kundi la watu waliojitolea na waajiriwa ambao huwezesha Makanisa na mashirika mbalimbali kuhudumia watu wenye uhitaji.

Baptist churches of various sizes and locations minister to human need. In addition to meeting spiritual needs through evangelism and Christian nurture, churches meet other aspects of human hurt — physical, mental, emotional and social. Counseling for the distressed, food for the hungry, clothes for the poor, transportation for the disabled … the list of ministries is practically endless.

Taasis za Baptist hutoa huduma kwa wahitaji. Uanzishwaji wa mashule na vyuo mbalimbali vya Kibaptistili walianza kutoa huduma za wahitaji wa elimu kabla shule za serikali na vyuo vinavyofadhiliwa na waipa kodi kuweko. Taasis kwa ajili ya kuhudumia watoto yatima na watoto wenye mazingira magumu ni baadhi ya taasis za kwanza kabisa za Wabaptist. Wabaptist husaidia taasis ambazo zinalea watu wazima. Hospitali na vituo vya afya chini ya Baptist kupitia huduma za kijamii mbalimbali. Taasis nyingi kutoa wafanyakazi na waliojitolea kwenye kwenye maeneo mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa huduma hizo.

Mashirika ya Baptist ya aina mbalimbali yapo ili kuweza kutoa huduma za kusaidia wahitaji kwa njia mbalimbali. Mengine kati ya hayo husaidia wakati wa majanga ya nchi, kama vile mafuriko, upepo mkali, tetemeko la ardhi, ili kutoa msaada kwa majanga hayo. Hayo mashirika hutoa msaada wa vyakula, maji safi na salama, nguo na kusaidia kujenga makazi mapya na hata Makanisa. Mengine hutoa mafunzo mbalimbali kama vile mafunzo kwa wasiokuwa na ajira, na kutoa mafunzo kwa ambao hawajui kusoma wala kuandika. Baadhi ya haya mashirika hujitegemea, mengine hushirikiana na makundi mbalimbali ya dini na hata yasiyo ya dini.

Kanda  na Majimbo ya Makanisa yameanzisha hizi taasis na mashirika, hutoa fedha kwao ambazo hupatikana kutoka kwa watu mbalimbali na Kanisa lenyewe, ili kusaidia uendeshaji wa hizo huduma.

Hitimisho

Kutoa huduma mbalimbali ni jambo la maana sana kwenye maisha ya Wabaptist. Kwa kufuata mwongozo wa Kibiblia na kuwezeshwa na nguvu za Roho Mtakatifu, Wabaptist wamejitoa kutoa huduma kwa jina la Yesu ili kukutana na mahitaji ya kibinadamu, kwa watu wote na mahala popote kwa Utukufu wa Mungu Baba.

“Jamani, Wakristo, msipuuzie hili, naomba niwaeleze jinsi ya kudhihirisha dini yenu.
ishi kwa hilo! Ishi kwa hilo!”
Charles Hadden Spurgeon
Mchungaji wa Baptist , London, England, 1800