Wabaptisti’ Maagizo Makuu Mawili: Ubatizo na Meza ya Bwana

“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,

mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana
na Roho Mtakatifu.”
Mathayo 28:19

“….Ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu, Na hihi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
1 Wakorintho 11:23-25

Wakristo wa madhehebu mengine hufurahia ubatizo na meza ya Bwana kwa njia fulani. Imani ya Wabaptist juu ya ubatizo na meza ya Bwana ni tofauti na madhehebu mengine.

Hizi tofauti ni sehemu ya kuleta chachu ili kuonyesha upekee wa Wabaptist na ni sehemu ya ladha ya mafundisho na desturi zao.

Ubatizo na Meza ya Bwana ni Ishara

Wabaptist kwa kawaida hutumia neno “maagizo makuu” kuliko neno “sakramenti” wakimaanisha ubatizo na meza ya Bwana. Hata kama neno “sakramenti” linatumika, haina maana kwamba hayo yote mawili ni muhimu kwa ajili ya mtu kuupata wokovu.

Wabaptist wameendelea kusema kuwa ubatizo na meza ya Bwana ni ishara tu na sio muhimu kwa ajili ya kuupata wokovu. Hata hivyo ni mambo muhimu kwenye kwa destruri za Wabaptist na ibada.

Kwa sababu ubatizo na meza ya Bwana ni ishara tu, kutumia ishara sahihi ni jambo la muhimu. Ubatizo ni ishara ya kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu ambaye alisababisha kutuletea wokovu. Ubatizo pia ni ishara inayoonyesha kwamba mtu kwa njia ya imani yake kwa Kristo amefufuliwa kutoka kifo hadi kupata uzima na mtu huyo  ametambuliwa na kifo cha Kristo na kufufuka kwake (Warumi 6:3-5 ; Wakolosai 2:12)

Ni njia ya kumzamisha mtu kwenye maji mengi ndio ishara ya kufa, kuzikwa na kufufuka.

Lakini pia, kutumia njia sahihi wakati wa meza ya Bwana kwa kile kinachomaanisha kwenye Biblia ni jambo la muhimu. Yesu alishiliki meza ya Bwana ya Bwana wakati wa chakula chake cha mwisho akiwa na wanafunzi wake kama sehemu ya desturi ya Kiyahudi ya kushiriki Pasaka (Mathayo 26:26-30; Mark 14:22-26; Luke 22:14-20). Mkate usiotiwa chache na tunda za mzabibu vilikuwa sehemu ya chakula hicho. Yesu alieleza kuwa mkate ni ishara ya mwili wake na lile tunda la mzabibu ni ishara ya damu yake. Mkate usiotiwa chachu uliachilia usafi wa Kristo, kwa kuwa hakuwa mtenda dhambi (Waebrania 4:15) kwa hiyo mwili wake ulifanyika kuwa dhabihu iliyo safi na bila mawaa kwa ajili ya kutusafisha dhambi. Mvinyo wa tunda la mzabibu ni ishara ya kwamba damu yake Kristo ilimwagika kwa ajili ya dhambi zetu.

Wakati wa kushiriki mkate na kikombe, Wafuasi wa Kristo wanapaswa kukumbuka sadaka yake aliyoitoa pale Msalanani Kalvari alipotoa mwili wake na kumwaga damu kwa ajili ya dhambi zetu. Wabaptisti huamini kwamba Biblia inatufundisha kwamba vitu vilivyotumika wakati ule haukuwa mwili halisi na wala damu halisi ya Kristo.

Ni ishara za mwili wake na damu yake. Unaposhiriki kuula mkate na kunywa kwenye kikombe, sio kwamba mtu anashiriki kweli mwili halisi na damu halisi ya Kristo, bali ni nafasi ya kuonyesha utii kwa Kristo na kukumbuka alivyofanyika kuwa sadaka kwa ajili yetu, uwepo wake kati yetu na kurudi kwake mara ya pili (1 Wakorintho 11:24-28).

Ubatizo na Meza ya Bwana Sio Ishara  za Kawaida tu

Kuamini kwamba ubatizo na meza ya Bwana kuwa ni ishara haina maana kwamba imani ya Wabaptisti ni yenye mashaka. Wabaptist huamini kwamba haya yote mawili ni ishara kuu.

Ni za muhimu sana kwa sababu ya uasili wake wa Kimungu. Hazijatokana na binadamu bali na Mungu mwenyewe kwetu sisi ili zisaidie kuihubiri injili (1 Wakorintho 11:26) na kutufanya tuishi maisha ya utauwa (1 Wakorintho 10:16-33; 11:29).

Kitendo cha kubatizwa kinampa mtu uweza ambaye amebatizwa kushuhudia mbele za watu kwamba ameamini na kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake na amesamehewa dhambi zake. Mtu anayebatizwa anaweza kuelezea maana halisi ya wokovu na maana ya ubatizo.

Meza ya Bwana husaidia kutoa nafasi ya kufanya uinjilisti na kukua katika Kristo. Jambo la muhimu na endelevu zaidi ni kuonyesha upendo wa Mungu ambao aliweza hata kumtoa Yesu afanyike mfano kwa ajili ya sadaka ya dhambi zetu.hivyo meza ya Bwana hujulikana pia kama Komunyo.

Ubatizo na Meza ya Bwana Ni sawa na Imani zingine za Baptist

Imani hizi za Wabaptist juu ya ubatizo na meza ya Bwana hazijitegemee. Zina uhusiano wa karibu sana na pia  ni pamoja na mafundisho mengine mazuri ya Wabaptisti.

Ubatizo na meza ya Bwana vinahusiana. Wabaptist huamini kwamba meza ya Bwana anayepaswa kushiriki ni wale waliozaliwa mara ya pili na kubatizwa.

Wabaptist wamejenga imani zao kwenye msingi wa Biblia, pamoja na imani juu ya ubatizo na meza ya Bwana. Biblia imeandikwa kwamba Makanisa ya Agano Jipya walifanya ubatizo na meza ya Bwana, kwa kufuata huo utaratibu na kama ishara. Haya Makanisa yalitokana na watu ambao wameokolewa na kubatizwa. Wabaptist huamini kwamba hizo hatua zinapaswa kufuatwa hata leo hii.

Kwa kusadiki juu ya ukuu wa Kristo, Wabaptist msingi wa imani yao juu ya ubatizo na meza ya Bwana ni kwenye mafundisho ya Yesu. Wabaptist mara nyingi hutumia neno “maagizo makuu” wakimaanisha hizo imani kwa saababu zilitolewa na Yesu mwenyewe (Mathayo 28:19; Luka 22:19; 1 Wakorintho 11:24-25).

Wabaptisti husisitiza kwamba wokovu hupatikana kwa neema ya Mungu kupitia Kristo tu, sio kwa matendo (Waefeso 2:8-9). Hivyo basi, Wabaptist huweka bayana kwamba ubatizo na meza ya Bwana, kwa umuhimu wake, lakini sio njia ya kuupata wokovu.

Kwa sababu Biblia inasema wote waliomini katika Kristo ni makuhani (1 Petro 2:5; Ufunuo 5:10), hakuna haja ya kuwa na darasa la ukuhani ili kuelezea suala la ubatizo au meza ya Bwana. Japo kwa kawaida ni Mchungaji ndiyo aneruhusiwa kubatiza halafu baadae anafanya meza ya Bwana, lakini kila muumini wa Kanisa ambaye amepangwa anaweza kufanya. Kwenye meza ya Bwana, kila kuhani muumini, na sio mmoja tu anayeongoza, bali wote waweze kushiriki kuumega mkate na kukinywea kikombe.

Uwezo na uhuru wa roho vinahusiana na ubatizo na meza ya Bwana kwa maana ya kwamba kila mmoja anyeshiliki anapaswa kufanya hivyo kwa hiari yake, asilazimishwe. Wabaptist wakati wote wamesisitiza uhuru wa kuabudu, wakisisitiza kwamba siwepo mtu wa kulazimishwa kwenye masuala ya kidini, kama vile ubatizo na meza ya Bwana.

Uongozi shirikishi na uhuru wa Kanisa chini ya ukuu wa Kristo pia huhusiana na haya maagizo makuu. Kuhusu ubatizo, kila Kanisa la Kibaptist lina mamlaka ya kupanga lini na wapi ubatizo ufanyike. Kuhusu meza ya Bwana, kila kanisa huaamua ni nani ataongoza, na itashirikishwa mara ngapi kwa mfano kwa mwaka, na labda ni nani ataalikwa kushiriki. Jambo la mwisho la kualika wengine, Makanisa mengine yanatoa mkazo wa kushiriki meza ya Bwana kwa washiriki wa Kanisa husika tu, Makanisa mengine hualika Makanisa ambayo wana “imani moja na utaratibu” kuweza kushiriki pamoja nao. Wengine hujumuisha wote waliobatizwa, na wachache wanatoa nafasi kwa wale ambao wamemkiri Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao ila hawajabatizwa.

Hitimisho

Wabaptist huamini kwamba Yesu alitoa maagizo makuu mawili ili yafanyike ndani ya Kanisa; yaani ubatizo na meza ya Bwana.

Kila moja ya hizo imani ni ishara na zina umuhimu sana ndani yake kwa sababu zinaachilia ujumbe wa Wakristo wa neema na wokovu na kuwa sawa  na mafundisho mengine ya Kibaptist.

“Tunaamini kwamba Kristo aliacha sakramenti mbili kwa Kanisa ili kuziendeleza, ubatizo, na meza ya Bwana, na sifa za kimaandiko juu ya ubatizo ni pamoja na kutubu na imani, na kwamba unafanyika kwa kuzamishwa kwenye maji mengi tu, na kwamba ubatizo ni sharti la meza ya Bwana.”
Sehemu 8 Mafundisho ya Maisha
Umoja wa Wabaptist Majimbo, 1840